SERIKALI YATOA BILIONI 15/- KUNUNUA MAHINDI

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imeshatoa sh. bilioni 15 kwa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) ili kununua mahindi kutoka kwa wakulima. “Uzalishaji wa mahindi ni mkubwa lakini na sisi pia tumeimarisha hifadhi yetu ya Taifa ya chakula. NFRA tumeipa fedha za kwenda kununua mahindi kwa bei ya kumwezesha mkulima ili ajikimu hadi